TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

UTANGULIZI

Chuo cha maafisa tabibu Bumbuli  ni chuo kilichoundwa kwa malengo la kutoa mafunzo ya ubora wa juu kwa wataalamu wa afya .

Chuo kinamilikiwa na  DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI  – KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA na namba ya usajili REG/HAS/073. Kinapatikana manispaa ya Bumbuli mkoa wa Tanga .

Chuo cha maafisa tabibu Bumbuli kinakaribisha maombi ya nafasi za kazi kwa watanzania wenye sifa  kama ifuatavyo

Wakufunzi II (Medical Doctors). Nafasi 2

Sifa

Shahada ya udaktari( Doctor of Medicine [M.D]) kutoka Chuo Kikuu/ Taasisi yoyote inayotambuliwa na Serikali. Na uzoefu ya kufundisha katika chuo cha utabibu. GPA ya 3.5 itakuwa sifa ya nyongeza.

Majukumu ya kazi

Anawajibika kwa  Mkurugenzi,

 Majukumu ya Mkufunzi:

 • Kuandaa mihadhara kwa wanafunzi
 • Kuandaa notes za kujifunzia kwa wanafunzi
 • Kushiriki katika kutunga ,kusimamia na kusahihisha mitihani na majaribio
 • Kufanya kazi za kiutawala kama kutunza ya orodha ya kila mwanafunzi
 • Kushiriki katika utafiti na ………………….
 • Kushiriki katika kutengeneza mtaala
 • Kufanya majukumu mengine kama utakavyopangiwa na mkuu wako wa idara

Mhasibu Daraja la II  –Nafasi 1.

Sifa:-

 (i)Shahada ya uhasibu kutoka Chuo Kikuu/ Taasisi yoyote inayotambuliwa na Serikali.

Kazi za kufanya:-

 1. Kuandaa rejesta ya cheki
 2. Kuidhinisha hati za malipo.
 3. Kuandika taarifa ya mapato na matumizi ya mwezi.
 4. Kusimamia shughuli za uhasibu kwenye Kitengo cha Idara.
 5. Kufanya majukumu mengine kama utakavyopangiwa na mkuu wako wa idara
 6.  

Mwisho wa kutuma maombi: 15 Agosti, 2020

Kituo cha kazi: Tanzania, Lushoto -Tanga

Imetumwa; Ijumaa, July 31, 2020

NAMNA YA KUTUMA MAOMBI:

Andika barua ya maombi kwenda kwa :

Mkurugenzi,

COTC Bumbuli,

S.L.P 09,

Bumbuli Tanga.

Ambatanisha CV, Kopi ya cheti cha kuzaliwa and vyeti vya kitaaluma.

Tuma kwenda : bumbuli.cotc@yahoo.com

You need advice/you have any query? we are here for you